Native Bible

Luke 7:46 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hukunipaka mafuta kichwani mwangu, lakini yeye ameipaka miguu yangu manukato.

Luke 7:46 in English

Luke 7:46 · Berean Standard Bible

You did not anoint My head with oil, but she has anointed My feet with perfume.

Context

44Kisha akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, “Je, unamwona mwanamke huyu? Nilipoingia nyumbani mwako, hukunipa maji ya kunawa miguu yangu, lakini huyu ameninawisha miguu kwa machozi yake, na kunifuta kwa nywele zake. 45Hukunisalimu kwa busu, lakini huyu mwanamke hajaacha kuibusu miguu yangu tangu nilipoingia. 46Hukunipaka mafuta kichwani mwangu, lakini yeye ameipaka miguu yangu manukato. 47Kwa hiyo, nakuambia, dhambi zake zilizokuwa nyingi zimesamehewa, kwani ameonyesha upendo mwingi. Lakini yule aliyesamehewa kidogo, hupenda kidogo.” 48Kisha akamwambia yule mwanamke, “Dhambi zako zimesamehewa.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.