Luka 7:45
Luke 7:45 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hukunisalimu kwa busu, lakini huyu mwanamke hajaacha kuibusu miguu yangu tangu nilipoingia.
Luke 7:45 in English
Luke 7:45 · Berean Standard Bible
You did not greet Me with a kiss, but she has not stopped kissing My feet since I arrived.
Context
43Simoni akajibu, “Nadhani ni yule aliyesamehewa deni kubwa zaidi.”
Naye Yesu akamwambia, “Umehukumu kwa usahihi.” 44Kisha akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, “Je, unamwona mwanamke huyu? Nilipoingia nyumbani mwako, hukunipa maji ya kunawa miguu yangu, lakini huyu ameninawisha miguu kwa machozi yake, na kunifuta kwa nywele zake. 45Hukunisalimu kwa busu, lakini huyu mwanamke hajaacha kuibusu miguu yangu tangu nilipoingia. 46Hukunipaka mafuta kichwani mwangu, lakini yeye ameipaka miguu yangu manukato. 47Kwa hiyo, nakuambia, dhambi zake zilizokuwa nyingi zimesamehewa, kwani ameonyesha upendo mwingi. Lakini yule aliyesamehewa kidogo, hupenda kidogo.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.