Native Bible

Luke 5:33 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakamwambia Yesu, “Wanafunzi wa Yohana na wa Mafarisayo mara kwa mara hufunga na kuomba, lakini wanafunzi wako wanaendelea kula na kunywa.”

Luke 5:33 in English

Luke 5:33 · Berean Standard Bible

Then they said to Him, “John’s disciples and those of the Pharisees frequently fast and pray, but Yours keep on eating and drinking.”

Context

31Yesu akawajibu, “Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio wagonjwa. 32Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu.” 33Wakamwambia Yesu, “Wanafunzi wa Yohana na wa Mafarisayo mara kwa mara hufunga na kuomba, lakini wanafunzi wako wanaendelea kula na kunywa.” 34Yesu akawajibu, “Je, mnaweza kuwafanya wageni wa bwana arusi kufunga wakati yuko pamoja nao? 35Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kwao. Hapo ndipo watakapofunga.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.