Native Bible

Luke 5:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yesu akawajibu, “Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio wagonjwa.

Luke 5:31 in English

Luke 5:31 · Berean Standard Bible

Jesus answered, “It is not the healthy who need a doctor, but the sick.

Context

29Kisha Lawi akamfanyia Yesu karamu kubwa nyumbani kwake, nao umati mkubwa wa watoza ushuru na watu wengine walikuwa wakila pamoja nao. 30Lakini Mafarisayo na walimu wa sheria waliokuwa wa dhehebu lao wakawalalamikia wanafunzi wa Yesu, wakisema, “Mbona mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na ‘wenye dhambi’?” 31Yesu akawajibu, “Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio wagonjwa. 32Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu.” 33Wakamwambia Yesu, “Wanafunzi wa Yohana na wa Mafarisayo mara kwa mara hufunga na kuomba, lakini wanafunzi wako wanaendelea kula na kunywa.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.