Luka 3:6
Luke 3:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nao watu wote watauona wokovu wa Mungu.’ ”
Luke 3:6 in English
Luke 3:6 · Berean Standard Bible
And all humanity will see God’s salvation.’”*
Context
4Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya:
“Sauti ya mtu aliaye nyikani,
‘Itengenezeni njia ya Bwana,
yanyoosheni mapito yake. 5Kila bonde litajazwa,
kila mlima na kilima vitashushwa.
Njia zilizopinda zitanyooshwa,
na zilizoparuza zitasawazishwa. 6Nao watu wote watauona
wokovu wa Mungu.’ ” 7Yohana akauambia ule umati wa watu uliokuwa unakuja ili kubatizwa naye, “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja? 8Basi zaeni matunda yastahiliyo toba. Wala msianze kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Abrahamu, baba yetu.’ Kwa maana nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Abrahamu watoto kutoka mawe haya.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.