Native Bible

Luke 23:45 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

kwa sababu jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likachanika vipande viwili.

Luke 23:45 in English

Luke 23:45 · Berean Standard Bible

The sun was darkened,* and the veil of the temple was torn down the middle.

Context

43Yesu akamjibu, “Amin, nakuambia, leo hii utakuwa pamoja nami Paradiso.”* 44Ilikuwa kama saa sita mchana, nalo giza likafunika nchi yote hadi saa tisa, 45kwa sababu jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likachanika vipande viwili. 46Yesu akapaza sauti yake akasema, “Baba, mikononi mwako naikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho. 47Yule jemadari alipoona yaliyotukia, akamsifu Mungu, akasema, “Hakika, mtu huyu alikuwa mwenye haki.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.