Luka 2:5
Luke 2:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Alikwenda huko kujiandikisha pamoja na Maria, ambaye alikuwa amemposa naye alikuwa mjamzito.
Luke 2:5 in English
Luke 2:5 · Berean Standard Bible
He went there to register with Mary, who was pledged to him in marriage and was expecting a child.
Context
3Kila mtu alikwenda kuandikishwa katika mji wake alikozaliwa. 4Hivyo Yosefu akapanda kutoka mji wa Nazareti ulioko Galilaya kwenda Uyahudi, mpaka Bethlehemu, mji wa Daudi, kwa sababu yeye alikuwa wa ukoo na wa nyumba ya Daudi. 5Alikwenda huko kujiandikisha pamoja na Maria, ambaye alikuwa amemposa naye alikuwa mjamzito. 6Wakiwa Bethlehemu, wakati wa Maria wa kujifungua ukawa umetimia, 7naye akamzaa mwanawe, kifungua mimba. Akamfunika nguo za kitoto na kumlaza katika hori ya kulia ngʼombe, kwa sababu hapakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.