Luka 2:10
Luke 2:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini malaika akawaambia: “Msiogope. Kwa maana tazama nawaletea habari njema za furaha itakayokuwa kwa watu wote.
Luke 2:10 in English
Luke 2:10 · Berean Standard Bible
But the angel said to them, “Do not be afraid! For behold, I bring you good news of great joy that will be for all the people:
Context
8Katika eneo lile walikuwako wachungaji waliokuwa wakikaa mashambani, wakilinda makundi yao ya kondoo usiku. 9Ghafula tazama, malaika wa Bwana akawatokea, nao utukufu wa Bwana ukawangʼaria kotekote, wakaingiwa na hofu. 10Lakini malaika akawaambia: “Msiogope. Kwa maana tazama nawaletea habari njema za furaha itakayokuwa kwa watu wote. 11Leo katika mji wa Daudi kwa ajili yenu amezaliwa Mwokozi, ndiye Kristo* Bwana. 12Hii ndiyo itakayokuwa ishara kwenu: Mtamkuta mtoto mchanga amefunikwa nguo za kitoto na kulazwa katika hori ya kulia ngʼombe.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.