Luka 18:41
Luke 18:41 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Unataka nikufanyie nini?” Akajibu, “Bwana, nataka kuona.”
Luke 18:41 in English
Luke 18:41 · Berean Standard Bible
“What do you want Me to do for you?” “Lord,” he said, “let me see again.”
Context
39Wale waliokuwa wametangulia mbele wakamkemea, wakamwambia akae kimya. Lakini yeye akapaza sauti zaidi, “Mwana wa Daudi, nihurumie!” 40Yesu akasimama, akawaamuru wamlete huyo mtu kwake. Alipokaribia, Yesu akamuuliza, 41“Unataka nikufanyie nini?”
Akajibu, “Bwana, nataka kuona.” 42Yesu akamwambia, “Basi upate kuona. Imani yako imekuponya.” 43Akapata kuona saa ile ile, akamfuata Yesu, huku akimsifu Mungu. Watu wote walipoona mambo hayo, nao wakamsifu Mungu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.