Luka 18:28
Luke 18:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo Petro akamjibu, “Tazama, tumeacha vyote tulivyokuwa navyo tukakufuata!”
Luke 18:28 in English
Luke 18:28 · Berean Standard Bible
“Look,” said Peter, “we have left all we had * to follow You.”
Context
26Wale waliosikia haya wakauliza, “Ni nani basi awezaye kuokoka?” 27Yesu akajibu, “Yasiyowezekana kwa wanadamu yanawezekana kwa Mungu.” 28Ndipo Petro akamjibu, “Tazama, tumeacha vyote tulivyokuwa navyo tukakufuata!” 29Yesu akajibu, “Amin, nawaambia, hakuna hata mtu aliyeacha nyumba yake, au mke, au ndugu, au wazazi au watoto kwa ajili ya Ufalme wa Mungu 30ambaye hatapewa mara nyingi zaidi ya hivyo katika maisha haya, na hatimaye kupata uzima wa milele ujao.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.