Luka 15:13
Luke 15:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Baada ya muda mfupi, yule mdogo akakusanya vitu vyote alivyokuwa navyo, akaenda nchi ya mbali, na huko akaitapanya mali yake kwa maisha ya anasa.
Luke 15:13 in English
Luke 15:13 · Berean Standard Bible
After a few days, the younger son got everything together and journeyed to a distant country, where he squandered his wealth in wild living.
Context
11Yesu akaendelea kusema: “Kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa na wana wawili. 12Yule mdogo akamwambia baba yake, ‘Baba, nipe urithi wangu.’ Hivyo akawagawia wanawe mali yake. 13“Baada ya muda mfupi, yule mdogo akakusanya vitu vyote alivyokuwa navyo, akaenda nchi ya mbali, na huko akaitapanya mali yake kwa maisha ya anasa. 14Baada ya kutumia kila kitu alichokuwa nacho, kukawa na njaa kali katika nchi ile yote, naye akawa hana chochote. 15Kwa hiyo akaenda akaajiriwa na mwenyeji mmoja wa nchi ile ambaye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.