Native Bible

Luke 13:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yesu alipomwona, akamwita, akamwambia, “Mwanamke, uwe huru, umepona ugonjwa wako.”

Luke 13:12 in English

Luke 13:12 · Berean Standard Bible

When Jesus saw her, He called her over and said, “Woman, you are set free from your disability.”

Context

10Basi Yesu alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo siku ya Sabato. 11Wakati huo huo akaja mwanamke mmoja aliyekuwa na pepo mchafu, naye alikuwa amepinda mgongo kwa muda wa miaka kumi na minane, wala alikuwa hawezi kunyooka wima. 12Yesu alipomwona, akamwita, akamwambia, “Mwanamke, uwe huru, umepona ugonjwa wako.” 13Yesu alipomwekea mikono yake, mara akasimama wima akaanza kumtukuza Mungu. 14Lakini kiongozi wa sinagogi akakasirika kwa sababu Yesu alikuwa ameponya mtu siku ya Sabato. Akaambia ule umati wa watu, “Kuna siku sita ambazo watu wanapaswa kufanya kazi. Katika siku hizo, njooni mponywe, lakini si katika siku ya Sabato.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.