Native Bible

Luke 11:37 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yesu alipomaliza kuzungumza, Farisayo mmoja alimwalika nyumbani mwake kwa chakula. Yesu akaingia na kuketi katika sehemu yake mezani.

Luke 11:37 in English

Luke 11:37 · Berean Standard Bible

As Jesus was speaking, a Pharisee invited Him to dine with him; so He went in and reclined at the table.

Context

35Kwa hiyo, hakikisha kwamba nuru iliyoko ndani yako isiwe giza. 36Basi ikiwa mwili wako wote umejaa nuru, bila sehemu yake yoyote kuwa gizani, basi utakuwa na nuru kama vile taa ikuangazavyo kwa nuru yake.” 37Yesu alipomaliza kuzungumza, Farisayo mmoja alimwalika nyumbani mwake kwa chakula. Yesu akaingia na kuketi katika sehemu yake mezani. 38Yule Farisayo akashangaa kwamba Yesu hakunawa kwanza kabla ya kula. 39Ndipo Bwana akamwambia, “Sasa, enyi Mafarisayo, mnasafisha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani mmejaa unyangʼanyi na uovu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.