Native Bible

Luke 11:35 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa hiyo, hakikisha kwamba nuru iliyoko ndani yako isiwe giza.

Luke 11:35 in English

Luke 11:35 · Berean Standard Bible

Be careful, then, that the light within you is not darkness.

Context

33“Hakuna mtu yeyote awashaye taa na kuiweka mahali palipofichika au kuifunikia chini ya bakuli. Badala yake huiweka juu ya kinara chake, ili watu wote wanaoingia waone nuru. 34Jicho lako ni taa ya mwili wako. Kama jicho lako ni zima, mwili wako wote pia umejaa nuru. Lakini kama jicho ni bovu, mwili wako wote pia umejaa giza. 35Kwa hiyo, hakikisha kwamba nuru iliyoko ndani yako isiwe giza. 36Basi ikiwa mwili wako wote umejaa nuru, bila sehemu yake yoyote kuwa gizani, basi utakuwa na nuru kama vile taa ikuangazavyo kwa nuru yake.” 37Yesu alipomaliza kuzungumza, Farisayo mmoja alimwalika nyumbani mwake kwa chakula. Yesu akaingia na kuketi katika sehemu yake mezani.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.