Native Bible

Luke 10:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akajibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote’; tena, ‘Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.’ ”

Luke 10:27 in English

Luke 10:27 · Berean Standard Bible

He answered, “‘Love the Lord your God with all your heart and with all your soul and with all your strength and with all your mind’* and ‘Love your neighbor as yourself.’*”

Context

25Wakati huo mtaalamu mmoja wa sheria alisimama ili kumjaribu Yesu, akamuuliza, “Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?” 26Yesu akamjibu, “Imeandikwaje katika Sheria? Kwani unasoma nini humo?” 27Akajibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote’; tena, ‘Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.’ ” 28Yesu akamwambia, “Umejibu vyema. Fanya hivyo nawe utaishi.” 29Lakini yule mtaalamu wa sheria, akitaka kujionyesha kuwa mwenye haki, akamuuliza Yesu, “Jirani yangu ni nani?”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.