Luka 10:1
Luke 10:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Baada ya hayo, Bwana akawachagua wengine sabini na wawili, akawatuma wawili wawili katika kila mji na kila sehemu aliyokusudia kwenda baadaye.
Luke 10:1 in English
Luke 10:1 · Berean Standard Bible
After this, the Lord appointed seventy-two * others and sent them two by two ahead of Him to every town and place He was about to visit.
Context
1Baada ya hayo, Bwana akawachagua wengine sabini na wawili, akawatuma wawili wawili katika kila mji na kila sehemu aliyokusudia kwenda baadaye. 2Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini watendakazi ni wachache. Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, ili apeleke watendakazi katika shamba lake la mavuno. 3Haya! nendeni. Ninawatuma kama wana-kondoo katikati ya mbwa mwitu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.