Luka 1:66
Luke 1:66 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kila aliyesikia habari hizi alishangaa akauliza, “Je, mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?” Maana mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.
Luke 1:66 in English
Luke 1:66 · Berean Standard Bible
And all who heard this wondered in their hearts and asked, “What then will this child become?” For the Lord’s hand was with him.
Context
64Papo hapo kinywa chake kikafunguliwa na ulimi wake ukaachiwa, akawa anaongea akimsifu Mungu. 65Majirani wote wakajawa na hofu ya Mungu, na katika nchi yote ya vilima vya Uyahudi watu walikuwa wakinena juu ya mambo haya yote. 66Kila aliyesikia habari hizi alishangaa akauliza, “Je, mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?” Maana mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye. 67Zekaria, baba yake, akajazwa na Roho Mtakatifu, naye akatoa unabii, akisema: 68“Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli,
kwa kuwa amewajilia watu wake na kuwakomboa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.