Walawi 9:11
Leviticus 9:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akateketeza nyama na ngozi nje ya kambi.
Leviticus 9:11 in English
Leviticus 9:11 · Berean Standard Bible
But he burned up the flesh and the hide outside the camp.
Context
9Wanawe wakamletea damu, naye akachovya kidole chake katika hiyo damu, akaitia kwenye pembe za madhabahu, nayo damu iliyobaki akaimwaga chini ya madhabahu. 10Juu ya madhabahu akateketeza mafuta, figo na mafuta yanayofunika ini kutoka kwenye hiyo sadaka ya dhambi, kama Bwana alivyomwagiza Mose. 11Akateketeza nyama na ngozi nje ya kambi. 12Kisha Aroni akachinja sadaka ya kuteketezwa. Wanawe wakamletea damu, naye akainyunyiza pande zote za madhabahu. 13Wakamletea sadaka ya kuteketezwa kipande kwa kipande, pamoja na kichwa, naye akaviteketeza juu ya madhabahu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.