Walawi 8:8
Leviticus 8:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akaweka kifuko cha kifuani juu yake, na kuweka Urimu na Thumimu* kwenye hicho kifuko.
Leviticus 8:8 in English
Leviticus 8:8 · Berean Standard Bible
Then he put the breastpiece on him and placed the Urim and Thummim * in the breastpiece.
Context
6Kisha Mose akamleta Aroni na wanawe mbele, akawaosha kwa maji. 7Akamvika Aroni koti, akamfunga mshipi, akamvika joho na kumvalisha kisibau. Pia akafunga kisibau juu yake na kukifunga kiunoni mwake kwa mshipi wake uliosokotwa kwa ustadi. 8Akaweka kifuko cha kifuani juu yake, na kuweka Urimu na Thumimu* kwenye hicho kifuko. 9Kisha akamvika Aroni kilemba kichwani pake, akaweka lile bamba la dhahabu, yaani ile taji takatifu, upande wa mbele wa kilemba, kama Bwana alivyomwagiza Mose. 10Ndipo Mose akachukua mafuta ya upako na kuipaka maskani na kila kitu kilichokuwamo ndani yake, kisha akaviweka wakfu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.