Walawi 8:10
Leviticus 8:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo Mose akachukua mafuta ya upako na kuipaka maskani na kila kitu kilichokuwamo ndani yake, kisha akaviweka wakfu.
Leviticus 8:10 in English
Leviticus 8:10 · Berean Standard Bible
Next, Moses took the anointing oil and anointed the tabernacle and everything in it; and so he consecrated them.
Context
8Akaweka kifuko cha kifuani juu yake, na kuweka Urimu na Thumimu* kwenye hicho kifuko. 9Kisha akamvika Aroni kilemba kichwani pake, akaweka lile bamba la dhahabu, yaani ile taji takatifu, upande wa mbele wa kilemba, kama Bwana alivyomwagiza Mose. 10Ndipo Mose akachukua mafuta ya upako na kuipaka maskani na kila kitu kilichokuwamo ndani yake, kisha akaviweka wakfu. 11Akanyunyiza baadhi ya mafuta juu ya madhabahu mara saba, akaipaka madhabahu mafuta na vyombo vyake vyote pamoja na sinia na kinara chake, ili kuviweka wakfu. 12Akamimina sehemu ya hayo mafuta ya upako kichwani mwa Aroni, akamtia mafuta ili kumweka wakfu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.