Native Bible

Leviticus 8:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kisha teketeza nyama na mikate iliyobaki.

Leviticus 8:32 in English

Leviticus 8:32 · Berean Standard Bible

Then you must burn up the remainder of the meat and bread.

Context

30Kisha Mose akachukua sehemu ya mafuta ya upako, na sehemu ya damu kutoka kwenye madhabahu, na kuvinyunyiza juu ya Aroni na mavazi yake, na juu ya wanawe na mavazi yao. Kwa hiyo akamweka Aroni na mavazi yake wakfu, pamoja na wanawe na mavazi yao. 31Kisha Mose akamwambia Aroni na wanawe, “Pika hiyo nyama kwenye ingilio la Hema la Kukutania, na uile hapo pamoja na mkate kutoka kwenye kikapu cha sadaka ya kuweka wakfu, kama nilivyoagiza, nikisema, ‘Aroni na wanawe wataila.’ 32Kisha teketeza nyama na mikate iliyobaki. 33Msitoke kwenye ingilio la Hema la Kukutania kwa muda wa siku saba, mpaka siku zenu za kuwekwa wakfu ziwe zimetimia, kwa kuwa muda wenu wa kuwekwa wakfu utakuwa siku saba. 34Lile lililofanyika leo liliagizwa na Bwana ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.