Walawi 8:31
Leviticus 8:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha Mose akamwambia Aroni na wanawe, “Pika hiyo nyama kwenye ingilio la Hema la Kukutania, na uile hapo pamoja na mkate kutoka kwenye kikapu cha sadaka ya kuweka wakfu, kama nilivyoagiza, nikisema, ‘Aroni na wanawe wataila.’
Leviticus 8:31 in English
Leviticus 8:31 · Berean Standard Bible
And Moses said to Aaron and his sons, “Boil the meat at the entrance to the Tent of Meeting and eat it there with the bread that is in the basket of ordination offerings, as I commanded, saying, ‘Aaron and his sons are to eat it.’
Context
29Kisha akachukua kidari, kilicho fungu la Mose la kondoo dume kwa ajili ya kuwekwa wakfu, na kukiinua mbele za Bwana kama sadaka ya kuinuliwa, kama Bwana alivyomwagiza Mose. 30Kisha Mose akachukua sehemu ya mafuta ya upako, na sehemu ya damu kutoka kwenye madhabahu, na kuvinyunyiza juu ya Aroni na mavazi yake, na juu ya wanawe na mavazi yao. Kwa hiyo akamweka Aroni na mavazi yake wakfu, pamoja na wanawe na mavazi yao. 31Kisha Mose akamwambia Aroni na wanawe, “Pika hiyo nyama kwenye ingilio la Hema la Kukutania, na uile hapo pamoja na mkate kutoka kwenye kikapu cha sadaka ya kuweka wakfu, kama nilivyoagiza, nikisema, ‘Aroni na wanawe wataila.’ 32Kisha teketeza nyama na mikate iliyobaki. 33Msitoke kwenye ingilio la Hema la Kukutania kwa muda wa siku saba, mpaka siku zenu za kuwekwa wakfu ziwe zimetimia, kwa kuwa muda wenu wa kuwekwa wakfu utakuwa siku saba.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.