Native Bible

Leviticus 7:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Paja la kulia la sadaka zako za amani utampa kuhani kama matoleo.

Leviticus 7:32 in English

Leviticus 7:32 · Berean Standard Bible

And you are to give the right thigh to the priest as a contribution from your peace offering.

Context

30Ataleta sadaka kwa mikono yake mwenyewe iliyotolewa kwa Bwana kwa moto; ataleta mafuta ya huyo mnyama pamoja na kidari, naye atainua hicho kidari mbele za Bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa. 31Kuhani atayateketeza hayo mafuta juu ya madhabahu, lakini kidari kitakuwa cha Aroni na wanawe. 32Paja la kulia la sadaka zako za amani utampa kuhani kama matoleo. 33Mwana wa Aroni atoaye damu na mafuta ya sadaka ya amani ndiye atakayepewa paja hilo la kulia kuwa fungu lake. 34Kutoka kwenye sadaka za amani za Waisraeli, mimi Mungu nimepokea kidari kile kilichoinuliwa pamoja na lile paja lililotolewa, nami nimevitoa kwa kuhani Aroni na wanawe kuwa fungu lao la kawaida kutoka kwa Waisraeli.’ ”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.