Native Bible

Leviticus 5:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Mtu anapokiuka na kutenda dhambi pasipo kukusudia kuhusu mojawapo ya mambo matakatifu ya Bwana, huyo mtu ataleta kwa Bwana kama adhabu kondoo dume mmoja kutoka kundi lake, asiye na dosari na mwenye thamani halisi kifedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Hii ni sadaka ya hatia.

Leviticus 5:15 in English

Leviticus 5:15 · Berean Standard Bible

“If someone acts unfaithfully and sins unintentionally against any of the LORD’s holy things, he must bring his guilt offering to the LORD: an unblemished ram from the flock, of proper value * in silver shekels according to the sanctuary shekel;* it is a guilt offering.

Context

13Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi yoyote ya hizo alizotenda, naye atasamehewa. Sadaka iliyobaki itakuwa ya kuhani, kama ilivyokuwa ile sadaka ya nafaka.’ ” 14Bwana akamwambia Mose: 15“Mtu anapokiuka na kutenda dhambi pasipo kukusudia kuhusu mojawapo ya mambo matakatifu ya Bwana, huyo mtu ataleta kwa Bwana kama adhabu kondoo dume mmoja kutoka kundi lake, asiye na dosari na mwenye thamani halisi kifedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Hii ni sadaka ya hatia. 16Ni lazima alipe kwa yale aliyoshindwa kufanya kuhusu vitu vitakatifu, kwa kuongeza sehemu ya tano ya thamani ile na kuitoa yote kwa kuhani, ambaye atamfanyia upatanisho kwa huyo kondoo dume kama sadaka ya dhambi, naye atasamehewa. 17“Kama mtu akifanya dhambi na kufanya yale yaliyokatazwa katika mojawapo ya amri za Bwana, hata ikiwa hajui, yeye ana hatia na anastahili adhabu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.