Walawi 26:10
Leviticus 26:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakati wa kuvuna mtakuwa bado mnakula mavuno ya mwaka uliopita, na itawalazimu kuyaondoa ghalani ili mpate nafasi ya mavuno mapya.
Leviticus 26:10 in English
Leviticus 26:10 · Berean Standard Bible
You will still be eating the old supply of grain when you need to clear it out to make room for the new.
Context
8Watu wenu watano watafukuza adui mia, watu wenu mia watafukuza adui elfu kumi, nao adui zenu wataanguka kwa upanga mbele yenu. 9“ ‘Nitawaangalia kwa upendeleo na kuwafanya mzae na kuzidisha idadi yenu, nami nitalishika Agano langu na ninyi. 10Wakati wa kuvuna mtakuwa bado mnakula mavuno ya mwaka uliopita, na itawalazimu kuyaondoa ghalani ili mpate nafasi ya mavuno mapya. 11Nitafanya makao yangu miongoni mwenu, nami sitawachukia. 12Nitatembea katikati yenu niwe Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.