Walawi 19:18
Leviticus 19:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“ ‘Usijilipizie kisasi wala kuwa na kinyongo dhidi ya mmoja wa jamaa yako, lakini mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Mimi ndimi Bwana.
Leviticus 19:18 in English
Leviticus 19:18 · Berean Standard Bible
Do not seek revenge or bear a grudge against any of your people, but love your neighbor as yourself.* I am the LORD.
Context
16“ ‘Usieneze uchochezi miongoni mwa watu wako.
“ ‘Usifanye kitu chochote kile kinachohatarisha maisha ya jirani yako. Mimi ndimi Bwana. 17“ ‘Usimchukie ndugu yako moyoni mwako. Karipia jirani yako kwa uwazi ili usishiriki hatia yake. 18“ ‘Usijilipizie kisasi wala kuwa na kinyongo dhidi ya mmoja wa jamaa yako, lakini mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Mimi ndimi Bwana. 19“ ‘Mtazishika amri zangu.
“ ‘Usiwaache wanyama wako wa kufugwa wakazaana na wengine wa aina tofauti.
“ ‘Usipande mbegu za aina mbili katika shamba lako.
“ ‘Usivae nguo iliyofumwa kwa nyuzi za aina mbili tofauti. 20“ ‘Kama mwanaume anakutana kimwili na mwanamke ambaye ni msichana mtumwa aliyeposwa na mwanaume mwingine, lakini ambaye hajakombolewa wala hajapewa uhuru, lazima iwepo adhabu inayofaa. Hata hivyo hawatauawa, kwa sababu msichana alikuwa bado hajaachwa huru.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.