Native Bible

Leviticus 19:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“ ‘Usiibe. “ ‘Usiseme uongo. “ ‘Msidanganyane.

Leviticus 19:11 in English

Leviticus 19:11 · Berean Standard Bible

You must not steal. You must not lie or deceive one another.

Context

9“ ‘Wakati uvunapo mavuno ya nchi yako, usivune hadi kwenye mipaka ya shamba lako, wala usikusanye mabaki ya mavuno yako. 10Usirudi mara ya pili katika shamba lako la mizabibu, wala usiokote zabibu zilizoanguka chini. Ziache kwa ajili ya maskini na mgeni. Mimi ndimi Bwana Mungu wako. 11“ ‘Usiibe. “ ‘Usiseme uongo. “ ‘Msidanganyane. 12“ ‘Usiape kwa uongo kwa Jina langu, na hivyo kulinajisi jina la Mungu wako. Mimi ndimi Bwana. 13“ ‘Usimdhulumu wala kumwibia jirani yako. “ ‘Usishikilie mshahara wa kibarua usiku kucha hadi asubuhi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.