Native Bible

Leviticus 18:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“ ‘Usikutane kimwili na mwanaume kama mtu akutanaye na mwanamke; hilo ni chukizo.

Leviticus 18:22 in English

Leviticus 18:22 · Berean Standard Bible

You must not lie with a man as with a woman; that is an abomination.

Context

20“ ‘Usikutane kimwili na mke wa jirani yako na kujitia naye unajisi. 21“ ‘Usimtoe mtoto wako yeyote awe kafara kwa mungu Moleki, kwani hutalinajisi kamwe jina la Mungu wako. Mimi ndimi Bwana. 22“ ‘Usikutane kimwili na mwanaume kama mtu akutanaye na mwanamke; hilo ni chukizo. 23“ ‘Usikutane kimwili na mnyama na kujitia unajisi kwake. Mwanamke asijipeleke kwa mnyama ili kukutana naye kimwili; huo ni upotovu. 24“ ‘Msijitie unajisi kwa njia yoyote katika hizi, kwa sababu hivi ndivyo mataifa nitakayoyafukuza mbele yenu yalivyojitia unajisi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.