Walawi 14:47
Leviticus 14:47 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yeyote atakayelala au kula ndani ya nyumba hiyo ni lazima afue nguo zake.
Leviticus 14:47 in English
Leviticus 14:47 · Berean Standard Bible
And anyone who sleeps in the house or eats in it must wash his clothes.
Context
45Ni lazima ibomolewe: mawe yake, mbao na lipu yake, vyote vikatupwe nje ya mji mahali palipo najisi. 46“Yeyote atakayeingia katika nyumba hiyo ikiwa imefungwa, atakuwa najisi mpaka jioni. 47Yeyote atakayelala au kula ndani ya nyumba hiyo ni lazima afue nguo zake. 48“Lakini ikiwa kuhani atakuja kuikagua na kukuta kuwa upele haujaenea tena baada ya nyumba kupigwa lipu, ataitangaza nyumba ile kuwa safi, kwa sababu upele umekwisha. 49Ili kuitakasa nyumba hiyo, mwenye nyumba ataleta ndege wawili, mti wa mwerezi, kitani nyekundu na hisopo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.