Walawi 13:29
Leviticus 13:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Ikiwa mwanaume au mwanamke ana kidonda juu ya kichwa au juu ya kidevu,
Leviticus 13:29 in English
Leviticus 13:29 · Berean Standard Bible
If a man or woman has an infection on the head or chin,
Context
27Siku ya saba kuhani atamchunguza tena, na kama unaenea kwenye ngozi, kuhani atamtangaza kuwa najisi; ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza. 28Lakini, kama alama ile haikubadilika na wala haijaenea kwenye ngozi, napo pamepungua, ni uvimbe kutokana na jeraha la moto, na kuhani atamtangaza kuwa safi; ni kovu tu kutokana na kuungua. 29“Ikiwa mwanaume au mwanamke ana kidonda juu ya kichwa au juu ya kidevu, 30kuhani atakichunguza kile kidonda, na kama ataona kuwa kimeingia ndani, na nywele zilizoko juu yake ni njano na nyembamba, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi, kwani ni upele; ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza wa kichwa au kidevu. 31Lakini kama kuhani akichunguza aina hii ya kidonda, kionekane kuwa hakina shimo na hakuna nywele nyeusi juu yake, basi atamtenga mtu huyo kwa siku saba.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.