Native Bible

Leviticus 13:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Bwana akawaambia Mose na Aroni,

Leviticus 13:1 in English

Leviticus 13:1 · Berean Standard Bible

Then the LORD said to Moses and Aaron,

Context

1Bwana akawaambia Mose na Aroni, 2“Iwapo mtu yeyote atakuwa na uvimbe au upele au alama nyeupe juu ya ngozi yake ambayo yaweza kuwa ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza,* ni lazima aletwe kwa Aroni kuhani ama kwa wanawe, kuhani mmojawapo. 3Kuhani atachunguza hicho kidonda kilichopo juu ya ngozi yake, na kama nywele za mahali palipo na kidonda zimebadilika kuwa nyeupe, na ikiwa kidonda kimeingia ndani ya ngozi, basi ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza, yaani ukoma. Kuhani atakapomchunguza, atamtangaza mtu huyo kuwa ni najisi kwa kawaida ya ibada.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.