Native Bible

Leviticus 13:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Iwapo mtu yeyote atakuwa na uvimbe au upele au alama nyeupe juu ya ngozi yake ambayo yaweza kuwa ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza,* ni lazima aletwe kwa Aroni kuhani ama kwa wanawe, kuhani mmojawapo.

Leviticus 13:2 in English

Leviticus 13:2 · Berean Standard Bible

“When someone has a swelling or rash or bright spot on his skin that could become an infectious skin disease,* he must be brought to Aaron the priest or to one of his sons who is a priest.

Context

1Bwana akawaambia Mose na Aroni, 2“Iwapo mtu yeyote atakuwa na uvimbe au upele au alama nyeupe juu ya ngozi yake ambayo yaweza kuwa ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza,* ni lazima aletwe kwa Aroni kuhani ama kwa wanawe, kuhani mmojawapo. 3Kuhani atachunguza hicho kidonda kilichopo juu ya ngozi yake, na kama nywele za mahali palipo na kidonda zimebadilika kuwa nyeupe, na ikiwa kidonda kimeingia ndani ya ngozi, basi ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza, yaani ukoma. Kuhani atakapomchunguza, atamtangaza mtu huyo kuwa ni najisi kwa kawaida ya ibada. 4Kama alama juu ya ngozi yake ni nyeupe, lakini haionekani kuwa imeingia ndani zaidi ya ngozi, na nywele kwenye alama hiyo hazijageuka kuwa nyeupe, kuhani atamtenga mtu huyo mahali pa pekee kwa siku saba.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.