Maombolezo 4:19
Lamentations 4:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Waliotufuatia walikuwa wepesi kuliko tai angani; walitusaka juu milimani na kutuvizia jangwani.
Lamentations 4:19 in English
Lamentations 4:19 · Berean Standard Bible
Those who chased us were swifter than the eagles in the sky; they pursued us over the mountains and ambushed us in the wilderness.
Context
17Zaidi ya hayo, macho yetu yalichoka,
kwa kutazamia bure msaada;
tuliangalia kutoka minara yetu
kwa taifa lisiloweza kutuokoa. 18Watu walituvizia katika kila hatua
hata hatukuweza kutembea katika barabara zetu.
Mwisho wetu ulikuwa karibu, siku zetu zilikuwa zimetimia,
kwa maana mwisho wetu ulikuwa umefika. 19Waliotufuatia walikuwa wepesi
kuliko tai angani;
walitusaka juu milimani
na kutuvizia jangwani. 20Mpakwa mafuta wa Bwana, pumzi ya uhai wetu hasa,
alinaswa katika mitego yao.
Tulifikiri kwamba chini ya kivuli chake
tungeliweza kuishi miongoni mwa mataifa. 21Shangilia na ufurahi, ee Binti Edomu,
wewe unayeishi nchi ya Usi.
Lakini kwako pia kikombe kitapitishwa,
Utalewa na kuvuliwa nguo ubaki uchi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.