Maombolezo 1:13
Lamentations 1:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kutoka juu alipeleka moto, akaushusha katika mifupa yangu. Aliitandia wavu miguu yangu na akanirudisha nyuma. Akanifanya mkiwa, na mdhaifu mchana kutwa.
Lamentations 1:13 in English
Lamentations 1:13 · Berean Standard Bible
He sent fire from on high, and it overpowered my bones. He spread a net for my feet and turned me back. He made me desolate, faint all the day long.
Context
11Watu wake wote wanalia kwa uchungu
watafutapo chakula;
wanabadilisha hazina zao kwa chakula
ili waweze kuendelea kuishi.
“Tazama, Ee Bwana, ufikiri,
kwa maana nimedharauliwa.” 12“Je, si kitu kwenu, ninyi nyote mpitao kando?
Angalieni kote mwone.
Je, kuna maumivu kama maumivu yangu
yale yaliyotiwa juu yangu,
yale Bwana aliyoyaleta juu yangu
katika siku ya hasira yake kali? 13“Kutoka juu alipeleka moto,
akaushusha katika mifupa yangu.
Aliitandia wavu miguu yangu
na akanirudisha nyuma.
Akanifanya mkiwa,
na mdhaifu mchana kutwa. 14“Dhambi zangu zimefungwa kwenye nira,
kwa mikono yake zilifumwa pamoja.
Zimefika shingoni mwangu
na Bwana ameziondoa nguvu zangu.
Amenitia mikononi mwa wale
ambao siwezi kushindana nao. 15“Bwana amewakataa wapiganaji wa vita
wote walio kati yangu,
ameagiza jeshi dhidi yangu
kuwaponda vijana wangu wa kiume.
Katika shinikizo lake la divai Bwana amemkanyaga
Bikira Binti Yuda.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.