Native Bible

Joshua 3:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Baada ya siku tatu maafisa wakapita katika kambi yote,

Joshua 3:2 in English

Joshua 3:2 · Berean Standard Bible

After three days the officers went through the camp

Context

1Yoshua na Waisraeli wote wakaondoka asubuhi na mapema kutoka Shitimu, wakaenda mpaka Mto Yordani, ambako walipiga kambi kabla ya kuvuka. 2Baada ya siku tatu maafisa wakapita katika kambi yote, 3wakitoa maagizo kwa watu, wakiwaambia: “Mtakapoona Sanduku la Agano la Bwana Mungu wenu, likichukuliwa na Walawi ambao ndio makuhani, mtaondoka hapo mlipo na kulifuata. 4Ndipo mtakapotambua njia mtakayoiendea, kwa kuwa hamjawahi kuipita kabla. Lakini msisogee karibu, bali kuwe na umbali wa dhiraa 2,000* kati yenu na Sanduku.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.