Yoshua 3:4
Joshua 3:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo mtakapotambua njia mtakayoiendea, kwa kuwa hamjawahi kuipita kabla. Lakini msisogee karibu, bali kuwe na umbali wa dhiraa 2,000* kati yenu na Sanduku.”
Joshua 3:4 in English
Joshua 3:4 · Berean Standard Bible
But keep a distance of about two thousand cubits * between yourselves and the ark. Do not go near it, so that you can see the way to go, since you have never traveled this way before.”
Context
2Baada ya siku tatu maafisa wakapita katika kambi yote, 3wakitoa maagizo kwa watu, wakiwaambia: “Mtakapoona Sanduku la Agano la Bwana Mungu wenu, likichukuliwa na Walawi ambao ndio makuhani, mtaondoka hapo mlipo na kulifuata. 4Ndipo mtakapotambua njia mtakayoiendea, kwa kuwa hamjawahi kuipita kabla. Lakini msisogee karibu, bali kuwe na umbali wa dhiraa 2,000* kati yenu na Sanduku.” 5Ndipo Yoshua akawaambia hao watu, “Jitakaseni, kwa kuwa kesho Bwana atatenda mambo ya kushangaza katikati yenu.” 6Yoshua akawaambia makuhani, “Liinueni Sanduku la Agano mkatangulie mbele ya watu.” Hivyo wakaliinua na kutangulia mbele yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.