Yoshua 24:29
Joshua 24:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Baada ya mambo haya, Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana akafa akiwa na umri wa miaka mia moja na kumi.
Joshua 24:29 in English
Joshua 24:29 · Berean Standard Bible
Some time later, Joshua son of Nun, the servant of the LORD, died at the age of 110.
Context
27Yoshua akawaambia watu wote, “Angalieni! Jiwe hili litakuwa shahidi juu yetu. Limesikia maneno yote Bwana aliyotuambia. Litakuwa shahidi juu yenu kama mtakuwa waongo kwa Mungu wenu.” 28Basi Yoshua akawatuma watu kila mmoja aende katika urithi wake mwenyewe. 29Baada ya mambo haya, Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana akafa akiwa na umri wa miaka mia moja na kumi. 30Nao wakamzika katika nchi ya urithi wake, huko Timnath-Sera* katika nchi ya vilima ya Efraimu, kaskazini ya Mlima wa Gaashi. 31Israeli wakamtumikia Bwana siku zote za maisha ya Yoshua, na za hao wazee walioishi baada ya Yoshua kufa, ambao waliona kila kitu Bwana alichowatendea Israeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.