Native Bible

Joshua 13:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yoshua alipokuwa mzee na umri wake ukiwa umesogea sana, Bwana akamwambia, “Wewe ni mzee sana, na bado kumesalia sehemu kubwa sana za nchi ambazo ni za kutwaliwa.

Joshua 13:1 in English

Joshua 13:1 · Berean Standard Bible

Now Joshua was old and well along in years, and the LORD said to him, “You are old and well along in years, but very much of the land remains to be possessed.

Context

1Yoshua alipokuwa mzee na umri wake ukiwa umesogea sana, Bwana akamwambia, “Wewe ni mzee sana, na bado kumesalia sehemu kubwa sana za nchi ambazo ni za kutwaliwa. 2“Nchi iliyosalia ni hii: maeneo yote ya Wafilisti na Wageshuri: 3kutoka Mto Shihori ulioko mashariki mwa Misri, kuelekea kaskazini kwenye eneo la Ekroni, ambayo yote ilihesabika kama ya Wakanaani (maeneo yale matano ya watawala wa Kifilisti, ambayo ni Gaza, Ashdodi, Ashkeloni, Gathi na Ekroni: ndiyo nchi ya Waavi);

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.