Yoshua 12:1
Joshua 12:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:
Joshua 12:1 in English
Joshua 12:1 · Berean Standard Bible
Now these are the kings of the land whom the Israelites struck down and whose lands they took beyond the Jordan to the east, from the Arnon Valley to Mount Hermon, including all the Arabah eastward:
Context
1Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba: 2Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.
Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi. 3Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi* hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi*), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.