Yoeli 3:9
Joel 3:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tangazeni hili miongoni mwa mataifa: Jiandaeni kwa vita! Amsha askari! Wanaume wote wapiganaji wasogee karibu na kushambulia.
Joel 3:9 in English
Joel 3:9 · Berean Standard Bible
Proclaim this among the nations: “Prepare for war; rouse the mighty men; let all the men of war advance and attack!
Context
7“Tazama nitawaamsha kutoka zile sehemu mlizowauza, nami nitawalipiza juu ya vichwa vyenu kile mlichofanya. 8Nitawauza wana wenu na binti zenu kwa watu wa Yuda, nao watawauza kwa Waseba, taifa lililo mbali.” Bwana amesema. 9Tangazeni hili miongoni mwa mataifa:
Jiandaeni kwa vita!
Amsha askari!
Wanaume wote wapiganaji
wasogee karibu na kushambulia. 10Majembe yenu yafueni yawe panga
na miundu yenu ya kukatia iwe mikuki.
Aliye dhaifu na aseme,
“Mimi nina nguvu!” 11Njooni haraka, ninyi mataifa yote kutoka pande zote,
kusanyikeni huko.
Shusha wapiganaji wako, Ee Bwana!
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.