Yoeli 2:21
Joel 2:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Usiogope, ee nchi; furahi na kushangilia. Hakika Bwana ametenda mambo makubwa.
Joel 2:21 in English
Joel 2:21 · Berean Standard Bible
Do not be afraid, O land; rejoice and be glad, for the LORD has done great things.
Context
19Bwana atawajibu:
“Ninawapelekea nafaka,
mvinyo mpya na mafuta,
vya kuwatosha ninyi
hadi mridhike kabisa;
kamwe sitawafanya tena
kitu cha kudharauliwa na mataifa. 20“Nitafukuza jeshi la kaskazini likae mbali nanyi,
nikilisukuma ndani ya jangwa,
askari wa safu za mbele wakienda
ndani ya bahari ya mashariki
na wale wa safu za nyuma
katika bahari ya magharibi.
Uvundo wake utapaa juu;
harufu yake itapanda juu.”
Hakika ametenda mambo makubwa. 21Usiogope, ee nchi;
furahi na kushangilia.
Hakika Bwana ametenda mambo makubwa. 22Msiogope, enyi wanyama pori,
kwa kuwa mbuga za malisho yenu
zinarudia ubichi.
Miti nayo inazaa matunda,
mtini na mzabibu inatoa utajiri wake. 23Furahini, enyi watu wa Sayuni,
shangilieni katika Bwana Mungu wenu,
kwa kuwa amewapa mvua za vuli
kwa kipimo cha haki.
Anawapelekea mvua nyingi,
mvua ya vuli na ya masika, kama mwanzoni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.