Yoeli 2:15
Joel 2:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Pigeni tarumbeta katika Sayuni, tangazeni saumu takatifu, liiteni kusanyiko takatifu.
Joel 2:15 in English
Joel 2:15 · Berean Standard Bible
Blow the ram’s horn in Zion, consecrate a fast, proclaim a sacred assembly.
Context
13Rarueni mioyo yenu
na siyo mavazi yenu.
Mrudieni Bwana, Mungu wenu,
kwa maana yeye ndiye mwenye neema
na mwingi wa huruma,
si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo,
huona huruma, hujizuia kuleta maafa. 14Ni nani ajuaye? Yeye aweza kugeuka na kuwa na huruma
na kuacha baraka nyuma yake:
sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji
kwa ajili ya Bwana Mungu wenu. 15Pigeni tarumbeta katika Sayuni,
tangazeni saumu takatifu,
liiteni kusanyiko takatifu. 16Wakusanyeni watu,
wekeni wakfu kusanyiko;
waleteni pamoja wazee,
wakusanyeni watoto,
wale wanyonyao maziwa.
Bwana arusi na atoke chumbani mwake
na bibi arusi naye atoke katika chumba chake. 17Makuhani, ambao wanahudumu mbele za Bwana,
na walie katikati ya ukumbi
wa Hekalu na madhabahu.
Waseme, “Wahurumie watu wako, Ee Bwana.
Usifanye urithi wako kitu cha kudharauliwa,
neno la dhihaka kati ya mataifa.
Kwa nini wasemezane miongoni mwao,
‘Yuko wapi Mungu wao?’ ”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.