Ayubu 42:14
Job 42:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Binti wa kwanza aliitwa Yemima, wa pili Kesia na wa tatu Keren-Hapuki.
Job 42:14 in English
Job 42:14 · Berean Standard Bible
He named his first daughter Jemimah, his second Keziah, and his third Keren-happuch.
Context
12Bwana akaibariki sehemu ya mwisho ya maisha ya Ayubu kuliko ile ya kwanza. Alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, ngamia elfu sita, jozi za mafahali elfu moja, na punda wa kike elfu moja. 13Tena alikuwa na wana saba na binti watatu. 14Binti wa kwanza aliitwa Yemima, wa pili Kesia na wa tatu Keren-Hapuki. 15Hapakuwepo mahali popote katika nchi ile yote palipopatikana wanawake wazuri kama binti za Ayubu; naye baba yao akawapa urithi pamoja na ndugu zao. 16Baada ya hili Ayubu akaishi miaka 140; akawaona wanawe na wana wa wanawe hata kizazi cha nne.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.