Native Bible

Job 4:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kama Mungu hawaamini watumishi wake, kama yeye huwalaumu malaika zake kwa kukosea,

Job 4:18 in English

Job 4:18 · Berean Standard Bible

If God puts no trust in His servants, and He charges His angels with error,

Context

16Yule roho akasimama, lakini sikuweza kutambua kilikuwa kitu gani. Umbo fulani lilisimama mbele ya macho yangu, kukawa na ukimya kisha nikasikia sauti: 17‘Je, binadamu aweza kuwa mwadilifu kuliko Mungu? Je, mtu aweza kuwa safi kuliko Muumba wake? 18Kama Mungu hawaamini watumishi wake, kama yeye huwalaumu malaika zake kwa kukosea, 19ni mara ngapi zaidi wale waishio katika nyumba za udongo wa mfinyanzi, ambazo misingi yake ipo mavumbini, ambao wamepondwa kama nondo! 20Kati ya mawio na machweo huvunjwa vipande vipande; bila yeyote kutambua, huangamia milele.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.