Native Bible

Job 33:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

kumwonea huruma na kusema, ‘Mwokoe asije akatumbukia shimoni; nimepata ukombozi kwa ajili yake’:

Job 33:24 in English

Job 33:24 · Berean Standard Bible

to be gracious to him and say, ‘Spare him from going down to the Pit; I have found his ransom,’

Context

22Nafsi yake inakaribia kaburi, nao uhai wake karibu na wajumbe wa kifo. 23“Kama bado kuna malaika upande wake kama mtetezi, mmoja miongoni mwa elfu, wa kumwambia mwanadamu lililo jema kwake, 24kumwonea huruma na kusema, ‘Mwokoe asije akatumbukia shimoni; nimepata ukombozi kwa ajili yake’: 25ndipo nyama ya mwili wake hufanywa mpya kama ya mtoto; hurudishwa upya kama siku za ujana wake. 26Humwomba Mungu, akapata kibali kwake, huuona uso wa Mungu na kushangilia kwa furaha; Mungu humrudisha katika hali yake ya uadilifu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.