Ayubu 3:23
Job 3:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa nini uhai hupewa mtu ambaye njia yake imefichika, ambaye Mungu amemzungushia boma?
Job 3:23 in English
Job 3:23 · Berean Standard Bible
Why is life given to a man whose way is hidden, whom God has hedged in?
Context
21wale wanaotamani kifo ambacho hakiji,
wale watafutao kufa zaidi ya kutafuta hazina iliyofichwa, 22ambao hujawa na furaha,
na hushangilia wafikapo kaburini? 23Kwa nini uhai hupewa mtu
ambaye njia yake imefichika,
ambaye Mungu amemzungushia boma? 24Kwa maana kulia kwangu kwa uchungu kwanijia badala ya chakula;
kusononeka kwangu kunamwagika kama maji. 25Lile nililokuwa naliogopa limenijia;
lile nililokuwa ninalihofia limenipata.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.