Native Bible

Job 29:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Utukufu wangu utabakia kuwa mpya ndani yangu, upinde wangu daima utaendelea kuwa mpya mkononi mwangu.’

Job 29:20 in English

Job 29:20 · Berean Standard Bible

My glory is ever new within me, and my bow is renewed in my hand.’

Context

18“Nikafikiri, ‘Nitafia katika nyumba yangu mwenyewe, nazo siku zangu zitakuwa nyingi kama chembechembe za mchanga. 19Mizizi yangu itafika mpaka kwenye maji, nao umande utakaa juu ya matawi yangu usiku kucha. 20Utukufu wangu utabakia kuwa mpya ndani yangu, upinde wangu daima utaendelea kuwa mpya mkononi mwangu.’ 21“Watu walinisikiliza kwa tumaini, wakingojea ushauri wangu kwa utulivu. 22Baada ya mimi kuzungumza, hawakusema zaidi; maneno yangu yaliingia masikioni mwao kwa makini.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.