Native Bible

Job 28:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hakuna ndege awindaye aijuaye njia ile iliyofichika, wala hakuna jicho la mwewe lililoiona.

Job 28:7 in English

Job 28:7 · Berean Standard Bible

No bird of prey knows that path; no falcon’s eye has seen it.

Context

5Ardhi, ambako chakula hutoka, chini hugeuzwa kwa moto; 6yakuti samawi hutoka katika miamba yake, nalo vumbi lake lina vipande vya dhahabu. 7Hakuna ndege awindaye aijuaye njia ile iliyofichika, wala hakuna jicho la mwewe lililoiona. 8Wanyama wa porini wanaotamba hawajawahi kupakanyaga, wala simba azungukaye huko. 9Mikono ya mwanadamu hushambulia miamba migumu sana, na kuiacha wazi mizizi ya milima.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.