Ayubu 28:6
Job 28:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
yakuti samawi hutoka katika miamba yake, nalo vumbi lake lina vipande vya dhahabu.
Job 28:6 in English
Job 28:6 · Berean Standard Bible
Its rocks are the source of sapphires, containing flecks of gold.
Context
4Huchimba shimo jembamba mbali na makao ya watu,
mahali paliposahaulika na nyayo za wanadamu;
mbali na wanadamu huningʼinia na kupembea kwa kamba. 5Ardhi, ambako chakula hutoka,
chini hugeuzwa kwa moto; 6yakuti samawi hutoka katika miamba yake,
nalo vumbi lake lina vipande vya dhahabu. 7Hakuna ndege awindaye aijuaye njia ile iliyofichika,
wala hakuna jicho la mwewe lililoiona. 8Wanyama wa porini wanaotamba hawajawahi kupakanyaga,
wala simba azungukaye huko.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.