Ayubu 24:19
Job 24:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kama vile joto na hari vinyakuavyo theluji iliyoyeyuka, ndivyo kuzimu kuwanyakuavyo waliotenda dhambi.
Job 24:19 in English
Job 24:19 · Berean Standard Bible
As drought and heat consume the melting snow, so Sheol steals those who have sinned.
Context
17Kwa wote hawa, giza nene ndiyo asubuhi yao;
hujifanya rafiki na vitisho vya gizani. 18“Lakini wao ni povu juu ya maji;
sehemu yao juu ya nchi imelaaniwa,
hivyo hakuna hata mmoja
aendaye kwenye shamba la mizabibu. 19Kama vile joto na hari vinyakuavyo theluji iliyoyeyuka,
ndivyo kuzimu kuwanyakuavyo waliotenda dhambi. 20Tumbo lililowazaa huwasahau,
nao huwa karamu ya mabuu;
watu waovu hawakumbukwi tena,
lakini huvunjika kama mti. 21Huwafanya mawindo wanawake tasa na wasio na watoto,
nao hawaonyeshi huruma kwa wajane.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.